Katika taarifa yao kuhusu Afrika, UNHCR ilieleza
kuwa Tanzania imewafukuza Wakimbizi wa Rwanda na Burundi katika operesheni ya
kuwaondoa Wahamiaji haramu inayoendelea nchini.
UNHRC
imeiomba radhi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia barua yake
ya tarehe 2 Oktoba, 2013.
Barua hiyo imeandikwa na Mkurugenzi wa UNHCR Kanda ya
Afrika Bw. George Okoth-Obbo kwenda kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhe. Pereira Ame Silima aliyeongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo
unaofanyika kila mwaka.
Katika barua hiyo, UNHCR imeeleza
kusikitishwa na taarifa hiyo ambayo si ya kweli na imekiri kwamba Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikishirikiana kwa karibu na UNHRC
katika ngazi zote kuhakikisha kwamba hakuna mkimbizi anayerejeshwa kwao katika
zoezi la kuwakamata na kuwarejesha kwao wahamiaji haramu linaloendelea nchini
Tanzania.
Aidha, Bw. Okoth Obbo ameeleza kuwa UNHCR na
Jumuiya ya Kimataifa kwa ujumla inatambua na kuthamini kwa dhati mchango mkubwa
ambao Tanzania imeutoa na inaendelea kuutoa katika kuwahifadhi wakimbizi wa
mataifa mbalimbali kwa kipindi cha takribani miaka 40.
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea kauli hiyo na kueleza kwamba
inatarajia na inaamini kwamba UNHCR itaendelea kutoa taarifa sahihi zenye kutoa
picha halisi inayoonesha namna Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
inavyotekeleza wajibu wake kuwalinda na kuwahifadhi Wakimbizi kwa mujibu wa
Sheria za nchi na mikataba ya Kimataifa ambayo nchi imeridhia.
Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
06,
Oktoba, 2013
0 comments:
Post a Comment