KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI .
“PRESS RELEASE” TAREHE 07. 10. 2013.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA MICHE YA
BHANGI.
MNAMO TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO
ENEO LA UYOLE JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA
JULIUS S/O MWAMBENJE, MIAKA 23, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA NSALAGA- UYOLE
AKIWA NA BHANGI MISOKOTO 15 SAWA NA UZITO WA GRAM 75. MBINU NI
KUFICHA BHANGI HIYO KWENYE MFUKO WA RAMBO. MTUHUMIWA NI MVUTAJI WA BHANGI.
TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA
WITO KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUINGIA NCHINI BILA KIBALI
MNAMO TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 23:30HRS HUKO
ENEO LA STENDI KUU JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA
WALIMKAMATA 1. NYELAKOZI D/O MELANIA, MIAKA 33,,MKULIMA, NA 2.
NDAISHIMILI D/O TEONYA,MIAKA 33,WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI BURUNDI
WAKIWA NA WATOTO 11 AMBAO PIA NI RAIA WA BURUNDI WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA
KIBALI. MBINU NI KUSAFIRI KWA NJIA YA KIFICHO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI
WAKABIDHIWE IDARA YA UHAMIAJI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII
KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA
SHAKA IKIWA NI PAMOJA NA WAHAMIAJI HARAMU ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE
DHIDI YAO.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA
MOSHI [GONGO]
MNAMO TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 08:30HRS HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA MAJENGO KIJIJI CHA LUPA WILAYA YA CHUNYA MKOA
WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA LYIDIA D/O AMBAKISYE, MIAKA
25, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA LUPA AKIWA NA POMBE HARAMU YA
MOSHI[GONGO] UJAZO WA LITA 5. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU
ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO
KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA
MOSHI [GONGO].
MNAMO TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 09:00HRS HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA MAGUNGA KIJIJI CHA MAMBA WILAYA YA CHUNYA MKOA
WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA JOHN S/O LUTIMBO, MIAKA 29,
MSUKUMA, MKULIMA, MKAZI WA MAMBA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO
WA LITA 4. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI
AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA
MATUMIZI YA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
0 comments:
Post a Comment