Hawa ni baadhi ya Watoto wakionekana wakiangalia banda la Vijana
kutoka mkoa wa Dar es salaam na bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na Vijana
hao leo katika viwanja vya Mlandege mkoani Iringa.
Hini ni viunga vya mji wa Iringa, Mkoa wa Iringa ambao ni Mwenyeji wa Wa Wiki ya Vijana Kitaifa, kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere na Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2013.
Hawa ni baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Iringa waliofika katika
banda la maonyesho la VETA mkoani Iringa hapa wakionekana wakipata maelezo ya bidhaa mbalimbali
zinazotengenezwa na na VETA kutoka kwa Bi. Oliva Adriano mwanafunzi wa mwaka wa
3 katika chuo cha Ufundi (VETA) mkoaani humo.
Askari wa Kikosi cha Zimamoto wakitoa elimu kwa baadhi ya
wakazi wa Iringa namna ya kutumia vifaa vya kuzimia moto na jinsi ya kukabiliana
na majanga ya moto katika maeneo yao wakati wa maonesho ya Wiki ya Vijana
Kitaifa yanayofanyika mkoani Iringa leo hii.
Vijana wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) katika mkoa wa Iringa
wakionyesha ujenzi wa nyumba za gharama nafuu wakati wa Maonyesho ya Wiki ya
Vijana Kitaifa mkoani Iringa .
0 comments:
Post a Comment