Mtuhumiwa mwenza wa Tukio hilo la Wizi,aliejitambulisha
kwa jina la Takula Manyenga mwenye umri wa Miaka 28,akidhibitiwa kwa kufungwa
kamba mara baada ya kukamatwa Usiku huu kwenye Hoteli ya Picolo,Kawe jijini Dar
es Salaam.
Watuhumiwa wote wawili wakipandishwa ndani ya Gari la Polisi
kutoka katika Kituo cha Kawe,Jijini Dar es Salaam.
Watuhumiwa hao wakiwa ndani ya gari la Polisi.
Askari Polisi wakiwa eneo la tukuo kuhakikisha Usalama
unapatikana eneo hilo.
Askari Polisi wakiwa na Watuhumiwa hao wakati wakiendelea
na Ukaguzi ndani ya Gari hilo aina ya Toyota Prado lenye nambari za Usajili T
445 BCY.
Askari Polisi wakiendelea na Ukaguzi ndani ya Gari
hilo,ambapo ndani ya Gari hilo kulikutwa na Simu zaidi ya kumi ambazo
zilichukuliwa na Polisi hao.
Gari walilokuwa wakilitumia
Watuhumiwa hao.
Wakipelekwa kwenye
Gari la Polisi tayari kwa safari ya kwenda Kituoni.
Ulinzi mkali kwa watuhumiwa hao.Msafara wa kuelekea kituoni.
Na.Mwandishi.
Watu wawili wanaosadikiwa kuwa
ni majambazi wamekamatwa usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya Picolo, Kawe
jijini Dar es Salaam wakati wakijaribu kutekeleza Azima yao.
Watu hao ambao wamekamatwa ni Bw. Takula
Mayenga mkazi wa Mbezi Temboni na Bw. Juma Hamis ambaye ni mkazi wa Tabata
wakiwa na nyaraka tofauti ikiwemo kitambulisho cha Idara ya Usalama wa Taifa,
kadi za benki pamoja na simu zaidi ya kumi,wakiwa katika harakati za kumtapeli
mwanadada mmoja aliejitambulisha kwa jina la Rebecca ambaye ni Mwanafunzi wa
Chuo cha Biashara cha CBE, Mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaa.
Akisimulia tukio dada huyo
ambaye alipatwa na tukio hilo la kutapeliwa Ijumaa ya wiki iliyopita alisema
kuwa, ilikuwa ni Ijumaa iliyopita wakiwa wamekaa katika fukwe wakipunga upepo
ndipo alipokuja tapeli huyo na kukaa nao na baadae aliwawekea madawa ya kulevya
na kuondoka na dada huyo kwenda kumtupa baharini.
JINSI MAJAMBAZI HAO WALIVYOKAMATWA;
Baada ya kuwa wamefanya tukio
Ijumaa ya wiki iliyopita la kumteka mwanadada na kumuibia vitu vyake vyote na
kisha kumtelekeza katika fukwe za bahari beach, na wao kuondoka.
Mwanadada huyo aliokolewa na
ndugu zake na kukutwa akiwa salama ila keshaibiwa vitu vingi sana ikiwemo siku.
Jukumu lililochukuliwa ni kwenda
katika mtandao wa tigo na kurejesha simu kadi yake na baada ya hapo waliomba
namba ya mwisho na kufanikiwa kupata namba ya huko tapeli.
Wanadada hao huku wakishirikiana
na familia kwa ujumla walichukua jukumu tena la kumpiga ile namba na kupokea
kaka ambaye wao walisema wamekosea namba na walikuwa wakimtaka mtu mwingine.
Jambazi hilo lilipoona namba
niya sauti ya mwanadada lilianza kumtongoza na kuomba miadi bila kujua lilikuwa
mtegoni. Mtego uliiva zaidi baada ya jamaa kupewa miadi ya kukutana hoteli ya
Piccolo na mwanadada aliyekuwa akiongea nae kwenye simu.
Jamaa bila kujua anaingia katika
mikono ya Polisi na wananchi wenye hasira kali alijongea mpaka hotelini pale na
kukutana na mwanadada ambaye aliyejitambulisha kuwa ndiye waliyeongea nae
kwenye simu.
Mtuhumiwa kwa ukarimu wake
alimuagizia mgeni wake kinywaji na kuanza maongezi, ndipo mtuhumiwa huyo
kuwekwa chini ya ulinzi na kutaka kukimbia huku mfukoni mwake akitoa
kitambulisho cha Idara ya Usalama wa Taifa na kukitupa na kuokotwa na wananchi
waliofika eneo la tukio.
Source/ Mwanajamii msikivu.
0 comments:
Post a Comment