Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Ndugu Mmari akimkabidi mfano wa hundi
yenye Barcode kwa ajili ya CD na nyimbo za mwanamuziki Pfofesa Jay huku wajumbe
wa Bodi ya GS1 Tanzania wakishuhudia.
Mwanamuziki Profesor Jay akiwa na mfano wa hundi yenye Barcode ambazo amekabidhiwa leo, Jay anakuwa mwanamuziki wa Pili kuchukua Barcode za Tanzania katika sekta ya muziki wa Bongo Fleva nchini.
.....................................................................................................................................................................
Na. Mwandishi Wetu.
Wanamuziki nchini Tanzania wametakiwa kuchangamkia mapema fursa zilizopo kwa kujitangaza na hatimaye kutanua wigo wa mashabiki wao
kwa kujiunga na huduma ya Barcode.
Kauli hiyo imetolewa na mwanamuziki mkongwe nchini Tanzania Profesa Jay wakati
alipokuwa akikabidhiwa Barcode kwa ajili ya CD yake mpya itakayojulikana kama
The Best of Professor Jay ambayo itakuwa na mchanganyiko wa nyimbo zake ambazo
zime heat tangu kuanza kwake.
“nimeamua kutoka kivingine na kwa sasa nataka
kufanya vitu kimataifa kwa kusambaza kazi zangu kwenye mitandao ili niwafikie
watu wengi zaidi” alisema Jay.
Katika makabidhiano hayo Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Bw. Elibariki Mmari alisema kuwa ni wakati muafaka kwa wanamuziki wa Tanznia kuanza kuuza kwenye mitandao ya kijamii na masoko ili soko la muziki liweze kutanuka zaidi kama wanavyofaidi fursa hizo wanamuziki wengine wa ndani na nje ya nchi.
Mmari alisema kutumia fursa hizo kwa
wanamuziki hao wanaweza kuuza kwenye mitandao ya kijamii kwa kupitia makampuni
makubwa duniani kama CD Baby ambalo lina mikataba na maduka yote makubwa ya
kwenye mtandao kama iTune, Facebook Music na mengine makubwa.
Hata hivyo Mmari aliongeza kwa kusema kuwa wanamuziki wa Tanzania hawawezi kuingia kwenye chati kubwa kama za Billboard bila kuwa na utambulisho wa ki electroniki wa Alama za Mistari yaani Barcode.
Kwa upande wake Afisa muandamizi wa GS1 Tanzania Bw.
Pius Mikongoti alisema kuwa ni vigumu kupata takwimu sahihi za usambazaji za
wanamuziki wa Tanzania kwani kazi zao haziko kwenye mfumo rasmi,
“ukiangalia
mwanamuziki kama Lady Jay Dee mathalani ana wafuasi wamefikia laki moja kwenye
mtandao wake wa kijamii wa Facebook kama atatangaza na kuuza kazi zake kwenye
mitandao hiyo ni wazi atawafikia Mashabiki wake kirahisi zaidi”
Takwimu za
Billboard zinachukuliwa kutokana na usambazaji na mauzo ya kazi za mwanamuziki
ki electroniki, ni vigumu kwa mwanamuziki kama Diamond ambaye kwa sasa ana
mashabiki lukuki na kazi zake kupigwa kila kona kupata takwimu sahihi za
usambazaji wake.
Pia amewataka wadau wa muziki nchini kuacha kusambaza nyimbo mpya za wanamuziki kwenye mitandao na kuwafanya watu waweze kuzipata bila kuzitolea chochote (downloads), kwa kufanya hivyo wanawaumiza sana wanamuziki wa Tanzania na kuwa hatuwasaidiii aliongeza Bw. Mikongoti.
Aidha GS1 Tanzania ndio watoaji pekee wa
huduma za BArcode kwa bidhaa zote za Tanzania, na ikumbukwe kuwa ili uweze kuuza
kwenye Supermarket na masoko ya mitandaoni ni lazima uwe na alama hizi za
mistari yaani Barcode.
0 comments:
Post a Comment