Tukio hilo lililotokea majira ya saa
moja na robo (1:15) za asubuhi ya leo, wakati gari hiyo iliyokuwa ikitokea
Tundauwa kwelekea mjini Chake Chake, iliposhindwa kupanda kilima cha Kunguni na
kurudi nyuma na kuanguka.
Majeruhi waliopokelewa katika hospitali ya
Chake Chake, ambao wamenusurika kifo ni pamoja na Salum Mohamed Salum (70),
Haji Salum Mohamed (23), Mzee Juma Saburi (50), Siti Massoud Dadi (60), Saidi
Seif Nassor (23).
Wengine ni Ameir Khatib (19), Suleiman
Ramadhan Aboud (23), Mariyam Khamis (32), Abdalla Suleiman Abrahman (30),
Zubeda Faki (38), Fatma Abeid Khamis (36), Amina Mohamed Abeid (40) na Abou
Abrahman Salum (67), wote ni wakaazi wa Kilindi.
Majeruhi wengine ni Fatma Ali Juma (70), Fatma
Khamis Ali wakaazi wa shengejuu, Nassor Abdalla Nassor (50) mkaazi wa Kungeni
na Rajab Ali Juma (43) mkaazi wa Tundauwa.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kanda wa
Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Saleh Mohamed Saleh alisema kuwa, gari hiyo
iyopata ajali ilikuwa ikiendeshwa na dereva Ali Salum Suleiman (25) mkaazi wa
Tundauwa.
Kamanda Saleh aliitaja gari hiyo yenye No Z884
BE yenyeruti Kilindi Chake, ilishindwa kupanda kilima cha Kunguni na kurudi nyuma
na kupinduka, huku dereva akishikiliwa na polisi.
Aidha alisema kuwa, katika majeruhi hao Tisa
mmoja kati yao Mzee Juma Saburi, amepelekwa Hospitali ya Mkoani
kwa matibabu zaidi baada ya kuumia mguu.
“Ajali imetokea kweli, bahati nzuri hakuna mtu
aliyepoteza maisha, ila majeruhi walichunika chunika kidogo katika sehemu za
kichwani, mikononi na kutibiwa na kuruhusiwa kwenda zao majumbani”alisema
kamanda Saleh.
Hata hivyo aliwataka madereva kuwa na
tahadhari sana wakati wanapoendesha gari zao, kwa kuziangalia kabla
ya kuanza safari, ili kuweza kuepuka ajili zisizokuwa za lazima.
0 comments:
Post a Comment