Image
Image

WATUMISHI NJE YA NCHI KUPATA MAFAO PSPF KUANZISHA UTARATIBU WA KUWASHIRIKISHA.


Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni PSPF, Adam Mayingu akitoa taarifa zamajukumu, mafanikio, changamoto na mipango ya mfuko kwa wadau wa mfukohuo waliohudhuria kwenye hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa naPSPF.

DAR ES SALAAM.
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma PSPF unatarajia kuwaingiza katika mpango wa mafao watumishi wa tanzania wanaofanya kazi nje ya nchi, ili kuwawezesha kupata mafao pindi wanapostaafu na kurejea nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Bw. Adam mahingu amefahamisha hayo wakati akizungumza wakati wa chakula cha Usiku, kilichoandaliwa kwa ajili ya wadau wa mfuko huo jijini Dar es Salaam.

Amesema watumishi hao wataingizwa kwenye mpango wa mafao chini ya utaratibu mpya ulioanzishwa wa uchangiaji wa hiyari, ambao umepanua wigo kwa kuruhusu wananchi wote hata walio nje ya utumishi wa umma kujiunga na mfuko huo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu huyo, Mfuko wa PSPF ambao ulianzishwa Julai 1999, umekuwa na kasi ya ukuaji wa asilimia 20 kwa mwaka ambapo hadi kufikia sasa umefanikiwa kuwa na amana zinazofikia thamani ya Shilingi Trilioni 1.25, zinazotokana na michango ya wanachama, uwekezaji na amana kwenye mabenki.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment