Meneja Masoko wa Bodi
ya Utalii (TTB) Bw. Geofrey Meena akitoa maelezo mbele ya waandishi wa habari
wakati akijibu maswali kwenye Warsha ya Mkakati wa kutangaza utalii wa Tanzania
kimataifa iliyoandaliwa na Boodi hiyo na kuhudhuriwa na wahariri na waandishi
mbalimbali wa vyombo vya habari pamoja na maafisa wa (TTB), Warsha hiyo
imefanyika leo kwenye hoteli ya New Africa leo jijini Dar es salaam. Kulia ni
Philip Chitaunga Meneja wa Huduma za Utalii (TTB) na kushoto ni Sam Kasulwa
Ofisa mawasiliano wa (Tourism Confederation of Tanzania
Ushauri huo
umetolewa leo jijini Dar es salaam na Meneja wa Huduma za Watalii kutoka Bodi
ya Utalii Tanzania TTB Bw. PHILLIP CHITAUNGA, alipokuwa akiwasilisha mada kwa
wahariri na waandishi wa habari , juu ya mkakati wa utangazaji wa Utalii
Tanzania na namna ya kuutangaza Utalii nje ya nchi.
Amesema Bodi
ya Utalii kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania TCT
wameazimia katika kutekeleza mkakati wa miaka mitano ijayo, watashirikiana kwa
karibu na sekta binafsi , sekta za umma , pamoja na vyombo vya habari
kuhakikisha wanatumia fursa zilizopo kuutangaza utalii , hivyo TTB na TCT
wameiomba jamii kushiriki pia kikamilifu kuutangaza utalii wa Tanzania.
Amesema hivi
sasa sekta ya Utalii inaingiza kiasi cha Dola za Kimarekani Bil. 1.7 kwenye
uchumi wa nchi na kwamba katika kuhakikisha mkakati waliojiwekea unaimarika
zaidi, TTB na TCT wameboresha mfumo wa utangazaji wa utalii kwa kutumia njia
mbalimbali za mawasiliano zikiwemo vipeperushi,mitandao ya kijamii, na kwenye
mikutano ya kimataifa.
Tayari Bodi
ya Utalii Tanzania imeshaanza kukutana na makundi mbalimbali ya wananchi pamoja
na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini ili kuhamasisha wananchi kuwa wazalendo katika kuutangaza
Utalii wa Tanzania ikizingatiwa kuwa hivi sasa utangazaji wa utalii ni wa watu
wote kutokana na umuhimu wake.









0 comments:
Post a Comment