Edward Lowassa.
Dar Es Salaam.
Licha jitihada kubwa zinayofanywa na serikali kwaajili ya kuhakikisha kuwa na ongezeko la shule na vyuo,
bado zipo changamoto kubwa zinazolikabili taifa ya namna ya kuhakikisha ubora wa
elimu inayotolewa kwenye shule na vyuo hivyo inaweza kumkomboa wananchi na
kumwezesha kukabiliana na changamoto za kimaisha.
Waziri mkuu mstaafu ambe pia ni mbunge wa Monduli Edward
Lowassa Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa harambee ya kuchangia mfuko wa elimu na ujenzi wa shule ya
awali inayotarajiwa kujengwa na kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama, kwa
shilingi millioni mia mbili hamsini zikiwa gharama za awali.
Amesema wakati nchi ipo katika mjadala wa namna ya kuboresha elimu nchini,
inatia moyo kuona wengine wameamua kutekeleza mjadala huo kwa vitendo na
kuongeza kuwa ukombozi wa kweli wa mtanzania utapatikana pale tu uhakika wa
kupata elimu bora utakapofanikiwa.
Kupitia mfuko
wa elimu wa usharika wa Kijitonyama matarajio ni kujenga shule ya awali katika
eneo hilo la kanisa, pamoja na kujenga shule ya msingi na sekondari ambapo eneo
limepatikana maeneo ya Maguepande Kinondoni jijijni dar es salaam.
Katika
harambee hiyo jumla ya shilingi millioni 615 zimepatikana ambapo Bwana Lowassa
na rafiki zake wamechangia jumla ya shilingi millioni sitini.
0 comments:
Post a Comment