STAA anayefanya vyema katika tasnia
ya filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper ameamua kurudi katika imani yake ya
awali ya Kikristo ikiwa ni miezi michache tangu alipotangaza kubadili dini na
kuwa Muislamu.
Novemba 3, mwaka huu (Jumapili
iliyopita) paparazi wetu alimnasa Wolper katika Kanisa la KKKT lililopo
Kijitonyama jijini Dar, akisali sambamba na waumini wa kanisa hilo.
Bila ya kificho, Wolper ambaye
alipokuwa Muislamu alikuwa akitumia jina la Ilham alisimama na kujitambulisha
kama muumini mpya wakati mchungaji wa kanisa hilo alipowataka waumini wapya
kufanya hivyo.
Wakati ibada hiyo ikiendelea, Wolper
alionekana kuimba pambio kwa hisia kali na ibada ilipoisha, alitoka kanisani
huku mkononi mwake akiwa ameshika Biblia.
Paparazi wetu alimfuata
Wolper na kumuuliza kilichomfanya arudi kwenye dini yake ya awali, naye alisema kwamba
amefanya hivyo kutokana na msukumo wa wazazi wake ambao kwa muda mrefu walikuwa
wakipinga kitendo chake cha kuwa Muislamu.
“Nimeamua kuurudia Ukristo kwa kuwa wazazi wangu kwa muda mrefu
walikataa mimi kuwa Muislamu, kwa hiyo kuanzia sasa siyo Ilham tena, niite
Jacqueline kama zamani,” alisema Wolper.
Mwaka
jana, Wolper alibadili dini na kuwa Muislamu kutokana na kuwa na uhusiano na
Abdallah Mtoro ‘Dallas’. Dallas akiwa nje ya nchi akamtaka Wolper kubadili dini
ili akirudi wafunge ndoa ya Kiislamu, Wolper alikubali naacqueline Wolper (kulia),
akiingia kanisani na rafiki yake kipenzi
kufanya
hivyo katika Msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni jijini Dar na kuchagua jina
la Ilham. Dallas alirudi nchini lakini wawili hao hawakufunga ndoa bali penzi
lao likaingia doa na kumwagana, Wolper akaendelea na msimamo wa imani yake hiyo
mpya na mara kwa mara alikuwa akidai kwamba hataiacha dini hiyo pamoja na
kumwagana na Dallas
0 comments:
Post a Comment