Mama Aisha Bilal
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Aisha
Bilal, anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye onesho la Usiku wa Khanga za Kale
2013 ‘5th Extra Vaa Khanga Party’ ndani ya Hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam, Novemba 8.
Mwandaaji wa onyesho
hilo, Asia Idarous, alisema usiku huo Mama Asha Bilal atakuwa mgeni rasmi
sambamba na watu mbalimbali maalufu wa ndani na nje ya Tanzania ambo pia
watashuhudia muziki wa bendi ya Mashauzi Classic na DJ Mkongwe nchini DJ John
Dilinga .
“Wadau wa mitindo
watapata burudani na kufurahia mitindo ya khanga itakayoonyeshwa kwenye shoo
hiyo, hii si ya kukosa kwa mwaka huu,” alisema Asia Idarous.
Usiku huo vazi la khanga ndilo
litakuwa maalumu kwa wadau watakaohudhuria sambamba na kupinga matumizi ya dawa
za kulevya.
Onyesho la Usiku
wa Khanga za Kale 2013 ambalo mwaka huu limeandaliwa kwa ushirikiano wa Asia
Idarous na Fabak Fashions, linatarajiwa kuwa na shangwe mbalimbali ikiwamo
kushirikisha watu maarufu na nyota mbalimbali.
Wakiwemo Shilole, Snura, Ben
Kinyaiya, Kibonde na wengineo.
Aidha,
alisema kati ya pesa zitakazo patikana pia zitaenda kusaidia kituo maalum cha
kupambana na waathirika wa dawa za kulevya.
Usiku wa Khanga za Kale umedhaminiwa na Redd’s, CXC, Clouds FM, Vayle
Spring, Magic FM, Eye View, Amina Design, Kabile, Vijimambo blog,Voice of
America, Origin Unite, Channel Ten, DTV, Times FM, Michuzi Media Group, Event
Light na Miss Tanzania,New Africa tv.com na wengine wengi.
0 comments:
Post a Comment