Mjane
wa Daudi Mwangosi Itika Mwangosi kulia akifuatilia
matukio yanayoendelea katika ukumbi huo.
Mhariri
wa magazeti ya New Habari (2006)Ltd Bw. Absalom Kibanda watatu kutoka kushoto
waliokaa mstari wa mbele aki bofya kifaa chake katika Tuzo hizo.
Na Mwandishi Wetu.
Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kujenga umoja
katika kupinga sheria kandamizi ya vyombo vya
habari na wanahabari nchini inayatarajia kupitishwa na
wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Meneja wa uthibiti wa ubora kutoka baraza la
habari Tanzania (MCT) Pili Mtambalike ametoa kauli hiyo leo
jijini Mwanza wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo
ya kishujaa na uandishi uliotukuka ya Daudi
Mwangosi .
Mtambalike amesema kuwa idadi ya
waandishi kutekwa na kuuwawa imezidi kuongezeka hapa
nchini huku kasi ya serikali kuvifungia vyombo
vya habari pia inaendelea kuongezeka .
Hivyo iwapo wanahabari nchini hawataungana
katika kupinga manyanyaso dhidi ya vyombo vya
habari na kupinga sheria kandamizi dhidi ya
vyombo vya habari na wanahabari suala la uhuru wa
vyombo vya habari nchini litaendelea kubaki ndoto.
Kwa upande wake rais wa umoja wa vilabu
vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Keneth Simbaya
alisema kuwa tuzo hiyo inayotolewa ni tuzo ya
kwanza kutolewa nchini Tanzania kwa waandishi
wanaopata matatizo wakati wanatekeleza wajibu wao.
Simbaya alisema kuwa UTPC imeamua kuanzisha
tuzo hiyo kama njia ya kuwapa moyo wanahabari
na kuuthibitishia umma kuwa wanahabari nchini
hawatakata tama katika kutumikia tasnia hiyo.
Alisema iwapo jamii inapaswa kujua ni vema
serikali kukubali kutoa habari kwa jamii inayopasa kujua
na inayo haki ya kupata habari.
“ Serikali itambue kuwa inapohitaji wananchi
kuchangia maendeleo ni vema itambue kuwa wananchi hao wana
haki ya kupata taarifa mbali mbali ya kile
walichochangia….ndani ya tukio la mauwaji ya Mwangosi
tumejifunza mambo mengi sana kwani tunapofanya kazi zetu wapo
wasiopenda kuona tunafanya kazi zetu hiyo”
Pia alisema ni vizuri wananchi kutambua kuwa
wakati wanahabari nchini wakitetea kupata habari
wasifikiri wanahabari wanajipangani wao .
Kwani alisema kuwa jitihada za
wanahabari kupigania uhuru wa kupata habari
zinapaswa kuungwa mkono na kila raia wa Tanzania ambayo ana
haki ya kupata habari.
Jaji mkuu wa tuzo hiyo Hamza Kasongo alisema kuwa
mchakato wa kumpata mshindi ulifanyika kwa kipindi cha
miezi miwili kuanza septemba hadi Octoba mwaka huu.
Tuzo hiyo ya uandishi wa habari wa
kishujaa na utumishi uliotukuka ya Daudi Mwangosi imetolewa
kwa Absalom Kibanda mhariri wa kampuni ya New habari (2006)
Ltd na mwenyekiti wa jukwaa la wahariri nchini (TEF).
0 comments:
Post a Comment