Wajumbe
wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya
Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN) wakiwa kwenye mazungumzo ya awali na
Mkuu wa Shule ya Arusha (Madam Kitigwa) baada ya kuwasili katika shule hiyo kwa
lengo la kukutana na Kilabu cha Umoja wa Mataifa shuleni hapo na kuzungumza na
Wanafunzi kuhusiana na agenda mbalimbali za Umoja huo.
Kituo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa kikishirikiana na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA)
wapo katika ziara ya kuzitembelea shule zenye na zisizo na Vilabu vya Umoja huo
kwa lengo la kufikisha habari na kazi za Umoja wa Mataifa.
Afisa
Habari wa Kituo cha Umoja Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza na
wanafunzi-wananchama wa klabu ya Umoja wa Mataifa katika Shule ya Msingi Arusha
Medium ambapo amewasisitiza juu ya umuhimu wa kuzifahamu agenda mbalimbali za
Umoja Mataifa na nafasi yao katika kuleta maendeleo chanya kwa jamii.
Mwenyekiti
Taifa wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa Tanzania Bara na Visiwani (UNCTN) Bw.
Rahim Rajab Nasser akizungumza na vijana wa shule ya msingi Arusha Medium juu
ya umuhimu wa vilabu hivyo na umuhimu wa ushiriki wao kuanzia shule za msingi
mpaka Sekondari na Vyuoni.
Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama
(katikati) akisisitiza jambo kwa vijana wa shule ya msingi Arusha Medium. Kulia
ni Mkutubi wa Maktaba ya kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi.
Harriet Macha na kushoto Mwenyekiti Taifa wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa
Tanzania Bara na Visiwani (UNCTN) Bw. Rahim Rajab Nasser.
Kobe
mwenye umri sawa na shule ya Msingi Arusha Medium iliyojengwa mwaka 1930 akiwa
hai mpaka na kuwa kivutio kwa wageni mbalimbali wanaofika shuleni hapo ikiwemo
Wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi
ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN).
Pichani
juu na chini ni baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha waliobahatika
kushiriki mkutano huo ulioendeshwa na Wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa
Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa
(YUNA/UNCTN).
Wajumbe
wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya
Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN) wakiwa na mwenyeji wa msafara wao MC
Kalinga wa Arusha wakielekea kukutana na wanafunzi wa Usa-River Academy
0 comments:
Post a Comment