Mhe. Balozi Mulamula akiingia ukumbini kwenye sherehe ya
kumkaribisha rasmi nchini Marekani iliyoandaliwa na jumuiya ya Watanzania DMV
siku ya Jumamosi Novemba 9, 2013 Lanham, Maryland na kuhudhuriwa na
Watanzania kutoka majimbo mbalimbali wakiwemo viongozi wa jumuiya ya New York.
Rais wa Jumuiya ya
Watanzania DMV bwn. Idd Sandaly akiongea na Watanzania na marafiki zao
waliofika kwenye sherehe ya kumkaribisha rasmi Balozi Mulamula siku ya jumamosi
Novemba 9, 2013 iliyofanyika Lanham, Maryland, machache aliyoongea Rais wa
jumuiya ni msisitizo wa Watanzania DMV kujiunga na jumuiya kwani umoja ni nguvu
na utengano ni udhaifu na baadae alimkaribisha Mhe. Balozi Liberata Mulamula.
Mhe. Balozi Liberata
Mulamula akicheza wimbo huku akisindikizwa na wakina mama na watoto wa darasa
la kiswahili DMV wakati alipokua akielekea kuongea na Watanzania waliofika
kumsikiliza.
Juu na chini ni Balozi Liberata Mulamula akiongea na Watanzania DMV siku
ya Jumamosi Novemba 9, 2013 Lanham, Maryland pamoja na mambo mengi aliyoongea
hotuba yake iliwasisimua wengi kiasi cha kumshangilia kwa wimbo wa "Balozi
sema, sema usiogope sema" alianza kwa kumsifia Balozi aliyepita Mhe.
Mwanaidi Maajar kwamba amevaa viatu vyake ambavyo kwake yeye ni vikubwa na
aliwaasa Watanzania kujiunga na jumuiya za Wanzania na kusisitiza wasigawanyike
kwa msingi ya tofauti zao za dini, itikadi au rangi na kuwaomba viongozi wa
jumuiya kuwa wabunifu wa mambo ya msingi ambayo yanamanufaa kwa Mtanzania
aishiye ughaibuni akatoa mfano wa Bima ya maisha na maswala ya uhamiaji huku
akisisitiza kwa kusema.
Juu na chini ni
Watanzania na marafiki zao wakimsikiliza mhe. Balozi wakati alipokua akiongea
na Watanzania kwenye sherehe ya kumkaribisha rasmi iliyoandaliwa na jumuiya ya
Watanzania DMV.
tusiwe wachoyo wakupeana siri za mafanikio ya mambo yenye manufaa na
yatakayomsaidia Mtanznia mwenzako, kama wewe
Juu na chini Balozi
Liberata Mulamula akipongezwa kwa hotuba yake nzuriiliyowagusa wengi aliyotoa
kwenye sherehe ya kumkaribisha rasmi iliyoandaliwa na jumuiya ya Watanzania
DMV.
0 comments:
Post a Comment