Mapinduzi
katika sekta ya kilimo yataweza kufanikiwa endapo wakulima kuanzia ngazi ya
chini hadi ya juu watawekewa bima katika kilimo chao itakayowasidia kuepuka
hasara inayosababishwa hasa na mabadiliko ya tabia nchi.
Ushauri huo
umetolewa jijini DSM na kamishna wa bima nchini, ISRAEL KAMUZORA wakati Wa
hafla ya kuanza ushirikiano wa kibiashara kati ya kampuni ya kimataifa ya bima
UAP na ya hapa nchini CENTURY, utakaowezesha wakulima wa ukanda wa afrika
mashariki kufaidika na huduma ya bima hatua itakayosaidia kukuza sekta hiyo
ambayo ndio uti wa mgongo wa taifa.
Awali
akizungumzia ubia huo wa utoaji huduma za bima katika ukanda wa nchi za afrika
mashariki,mkurugenzi mkuu wa UAP GROUP na mkurugenzi mkazi wa UAP CENTURY
wamedai kampuni hiyo kwa sasa imeanza na uwekezaji wa bilioni 9 na tayari ina
matawi 12 katika ukanda huo ambapo sekta ya kilimo,madini na maswala ya anga na
nyinginezo zitaweza kufaidika katika nchi hizo.
0 comments:
Post a Comment