Abdulaziz Ahmed- lindi.
=================
Wito
umetolewa kwa Serikali Nchini kutoa upendeleo wa Vifaa katika sekondari za Kata
ikiwemo upendeleo wa kupatiwa walimu wa kutosha wa masomo ya Sayansi ili
kusaidia Ukuaji wa Uchumi kwa wakazi wa Mikoa ya kusini ili waufaike na fursa
zilizopo kiuchumi.
Hayo
yamebainishwa katika Taarifa ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kineng'ene
iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, katika hafla fupi ya kupokea
Meza 2 za maabara zilizotolewa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)
zenye thamani zaidi ya Sh.11.99 milioni.
Taarifa hiyo
iliyosomwa na Mwalimu Esther Lumato imebainisha baadhi ya changamoto
zinazoikabili shule hiyo ikiwemo ukosefu wa umeme, hatua inayozorotesha ufanisi
katika masomo.
Naye, meneja
wa Mfuko wa NSSF mkoani Lindi, Bi Shani Mtani amewataka wanafunzi kutokubali
kudanganywa kwa vishawishi vyovyote badala yake wazingatie masomo hususani ya
Sayansi, kwani ndiyo yatakayowasaidia katika maisha yao ya baadae.
Awali akitoa
taarifa ya Elimu katika manispaa hiyo, Kaimu Afisa elimu sekondari, Maurus
Ndunguru alisema utoro bado ni changamoto kubwa Mkoani Lindi na kwamba kwa
wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu kati ya
wanafunzi 767 walioripoti hadi sasa ni wanafunzi 229 ikiwa sawa na 29.9%.
0 comments:
Post a Comment