Mkuu wa kitengo cha Maafa,ofisi ya Waziri Mkuu, Luteni Jenerali mstaafu, Sylvester Chacha Rioba akipokea msaada wa vitu mbali mbali kwa , Balozi wa China hapa nchini, Lu Youqing jijini Dar es salaam.
Ubalozi wa
China hapa nchini umetoa msaada wa kibinadamu wa vitu mbalimbali ikiwemo
vyakula, magodoro, mablanketi, nguo, mafuta wenye thamani ya shilingi milioni
30, kwa ajili ya waathirika wa mafuriko wilayani Mvomero mkoani Mororogo.
Akikabidhi
msaada huo jijini Dar es salaam, kwa mkuu wa kitengo cha Maafa, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Luteni Jenerali mstaafu, Sylvester Chacha Rioba, Balozi wa China hapa
nchini, Lu Youqing amesema Tanzania na China zina udugu wa kihistoria na
kuongeza kwamba maafa yaliyotokea Morogoro yamewagusa wananchi wa China kwa
kiasi kikubwa.
Amesema ana
imani katika uongozi madhubuti wa Rais Jakaya Kikwete, wananchi wa Morogoro
waliokumbwa na mafuriko watavuka vyema katika kipindi hiki kigumu na kujenga
upya maisha yao.
January 22
mwaka huu, mvua kubwa zisizotabirika kutokea milima ya Kilosa na Mvomero mkoani
Morogoro zilizasababisha mafuriko makubwa katika mto Mkundi, hali
iliyosababisha kukatika kwa daraja la Dumila ambalo linaunganisha barabara kuu
ya Dodoma na Morogoro.
0 comments:
Post a Comment