Jukwaa la
Kimataifa la Uchumi- WEF, limeteua mradi
wa ukanda wa uchukuzi wa kati mpaka upande wa Magharibi unaopakana na nchi
jirani, kama mradi wa mfano wa kuwekewa msukumo wa kifedha na kiteknolojia
katika utekelezaji wake, ili uwe mfano wa ushiriki wa sekta binafs katika
ujenzi wa miundo mbinu barani Afrika.
Mradi huo
utahusisha ujenzi wa Barabara, Reli na kuiboresha Bandari ya Dar es salaam kwa
manufaa ya mataifa ya Tanzania, na nchi jirani za upande wa magharibi na
kaskazini magharibi.
Katika
Mkutano wa WEF uliofanyika DAVOS nchini Uswisi, kuanzia januari 22 hadi 26
mwaka huu, kati ya miradi 51 ya bara la Afrika, mradi huo ambao kwa asilimia
tisini upo nchini Tanzania, ulichaguliwa kusaidiwa kifedha na kiutendaji ili
kuukamilisha, ambapo wiki ya kwanza ya mwezi April viongozi wa Umoja wa Afrika
wanatarajia kukutana nchini kwa lengo la kuweka mipango ya kuufanikisha.
Waziri wa
Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, ambaye alikuwa miongoni mwa ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na rais
Kikwete kwenye mkutano huo, ameelezea serikali inakusudia kuunda kamati yenye
wajumbe wanane kwa lengo la kusaidia kufanikisha mpango huo.
0 comments:
Post a Comment