Waziri Mkuu wa Finland JYRKI KATAINEN
Waziri Mkuu
wa Finland JYRKI KATAINEN ameishauri Mamlaka ya bandari kufanya kazi kwa
kuzingatia Usalama, ubora na uharaka ili kukuza ufanisi wa bandari hiyo.
Kauli hiyo ameisema wakati alipokuwa kizungumza
na watendaji wa mamlaka ya bandarai na maafisa wengine wa serikali mara baada
ya kutembelea bandari ya Dar es salaam, ambapo Bw Katainen amesema nchi yake ipo
tayari kuisaidia Tanzania katika juhudi zake za kuiboresha bandari hiyo iwe ya
kisasa.
Ujumbe wa
Tanzania katika mazungumzo na wenzao wa Finland, ulimwelezea Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Finland kuwa, baadhi ya changamoto zinazoikabali mamlaka ya bandari
nchini ni ukosefu wa rasailimali watu wenye ujuzi, teknolojia ya kupakia na
kupakua mizigo kwenye meli pamoja na maghala ya kisasa ya kuifahidhia mizigo.
Bandari ya
Dar es salaam imekuwa ikinunua baadhi ya vifaa na mitambo mikubwa ya
kubebea mizigo kutoka Finland, na pia
makampuni mawili makubwa ya taifa hilo la Ulaya Kaskazini yamekuwa yakitoa
huduma ya kusafirisha na kupokea mizigo yenye kemikali inayopitia bandarini
hapo.
Aidha bandari ya Dar es salaam imekuwa ikipitisha mizigo inayoingia na kutoka zaidi ya tani milion 13.5 kwa mwaka. Na imekuwa ikitumiwa na mataifa jirani kwa ajili ya kupitisha mizigo yao pia.
0 comments:
Post a Comment