WATU kumi na
watatu wamefariki dunia Mkoani Singida,wakiwemo watatu wa familia moja baada ya
gari aina ya Noah lenye namba za usajili Na.T730 BUX walilokuwa wakisafiria
kutoka Itigi kwenda Singida kugongwa na lori lenye namba za usajili T687 aina
ya AXB katika Kijiji cha Isuna,wilaya ya Ikungi,Mkoani Singida leo.
MGANGA
Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Singida,Dk.Deogratius Banuba amesema amepokea
miili kumi na mitatu ya marehemu hao ambapo kumi na mmoja wameshatambuliwa.
Baadhi ya
mashuhuda wamedai kuwa lori hilo lililokuwa likitokea Mkoani Mwanza kwenda Dar-es-Salaam likiwa na shehena ya
samaki liliacha njia na kuifuata Noah na kisha kuliparamia juu na hivyo
kusababisha vifo hivyo papo hapo.
Kamanda wa
polisi Mkoa wa Singida, SACP,Geofrey Kamwela amesema ajali hiyo imesababishwa
na mwendo kasi wa magari yote. Kwa mara nyingine ametoa wito kwa madereva kuwa
waangalifu wanapokuwa barabarani.
KATIKA mwezi
huu pekee wa Januari 2014, hiyo ni ajali ya pili mbaya kutokea Mkoani Singida
ambayo imesababisha vifo vya watu pamoja na majeruhi katika barabara kuu
itokayo Singida kwenda Dar-es-Salaam.
0 comments:
Post a Comment