Viongozi
mbalimbali duniani wanaendelea kutuma salamu zao za rambirambi kufuatia kifo
cha rais wa zamani wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela.
Katika salamu
zake za rambirambi, rais barack Obama wa Marekani amesema Mzee Mandela
aliibadilisha Afrika Kusini na kuuendesha ulimwengu na alipata mafanikio mengi
zaidi kuliko mtu mwingine yeyote na kuongeza kwamba dunia imepoteza mmoja wa
watu wenye ushawishi na ujasiri.
Mjini London,
waziri mkuu wa Uingereza bw. David Cameron ametuma salamu za rambirambi kwa
kusema Mzee Mandela ni miongoni mwa watu walioing'arisha zaidi dunia na kwamba
hakuwa tu shujaa wa kipindi kilichopita bali ataendelea kuwa shujaa wakati
wote.
Kansela wa
Ujeruani Angela Merkel amesema Mzee Mandela ni mfano wa ubinadamu ambaye sifa
yake itawapa moyo watu ulimwenguni kote huku katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Ban Ki Moon akimuelezea Mzee Mandela kama bingwa wa haki duniani.
Rais wa
zamani wa Marekani Bill Clinton, ambaye alikuwa madarakani Nelson Mandela
alipochukua urais nchini Afrika Kusini, ameomboleza kifo cha shujaa huyo kwa
kusema alikuwa "bingwa wa hadhi ya binadamu na uhuru".
0 comments:
Post a Comment