Image
Image

SIKU YABABA DUNIANI IPEWE KIPAO MBELE.

LEO Watanzania wanaungana na jamii ya kimataifa kuadhimisha Siku ya Baba ambayo huadhimisha Jumapili ya Tatu ya mwezi wa sita kila mwaka.

Siku hii haina tofauti na Siku ya Mama ambayo huadhimishwa Jumapili ya Pili ya mwezi wa tano kila mwaka. Lengo la Siku hii ya Baba ni kutafakari na kuwashukuru wazazi wa kiume kwa mchango wao wa hali na mali katika malezi ya watoto.

Kwa kuwa kila binadamu huzaliwa na baba na mama basi leo ni siku mahsusi ya kumshukuru baba yako au mlezi wa kiume kwa mchango wake katika maisha.

Ingawa tunapaswa kushukuru kila siku, leo ni siku maalum kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kutupatia baba au baba mlezi ambayo wamefanya mengi kuhakikisha kuwa watoto wanapata mahitaji maalum na malezi mazuri.

Pia leo ni siku muafaka kwa wazazi wa kiume kutafakari juu ya wajibu wao katika malezi ya watoto. Ni siku mahususi kwa akinababa kuwakumbuka watoto wao hasa wale waliozaliwa nje ya ndoa.

Pia akinamama wenye watoto waliozaliwa nje ya ndoa wanapaswa kutumia siku ya leo kuwakutanisha watoto hao na baba zao kwa sababu ni haki ya kila mtoto kumfahamu baba yake bila kujali wamezaliwa katika mazingira gani.

Enyi wazazi hebu wapatieni watoto wenu majibu maana kuna watoto wengi wanauliza, “baba uko wapi?...natamani kukuona ili nikushukuru kwa mchango wako katika maisha yangu.”

Akinababa mnapaswa kutenga muda wa kukaa na watoto wenu, kula na kunywa pamoja ili kuimarisha upendo katika familia. Ni vyema kujenga utamaduni wa kuwashukuru na kuwaenzi akinababa kwa sababu kila baba ana mchango katika maisha ya mtoto.

Kwa wale ambao baba zao wametangulia mbele za haki basi wanapaswa kuwaombea ili waweze kupumzika kwa amani.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment