Air Tanzania
|
Zaidi ya abiria mia moja wa ndege ya Air
Tanzania wamekwama nchini Tanzania, baada ya safari za shirika hilo la ndege
kuarishwa.
Wengi wa abiria hao walikua wakifanya
safari kuelekea nchini Comoros na wengine wakiwa katika safari za ndani,
wakielekea Mtwara na Kigoma, wamekwama kwa siku mbili mjini Dar es salaam.
kutokana na kadhia hiyo shirika hilo
lililazimika kukodi hoteli kuwahifadhi abiria hao kama ilivyo ada inapotokea
dharura wakisubiri muafaka wa namna watakavyosafiri kuelekea Comoro. Sharifu
Hashim, Balozi wa heshima wa Comoro huko Chicago nchini Marekani, anasema mambo
yake mengi yamekwama kutokana na tukio hili na hajapata uhakika ataondoka lini
Zenabal Mwarabu yeye hofu yake ni kwa namna
gani ataweza kuiwahi ndege aliyokuwa aunganishe Kisiwani Comoro kuelekea katika
kisiwa kingine cha Rarinyo.Msawi Seifu anasema ijapokuwa tatizo hili limetokea
lakini Air Tanzania ni mkombozi kwa wana Comoro.
Lily Fungamtama, Mkuu wa Kitengo cha Biashara
amesema tayari Air Tanzania inashughulika kuhakikisha abiria wote wanasafiri
mapema kesho .
Sikukuu za mwisho wa mwaka ndilo tatizo la
kukwama kwa abiria hao,kwani marubani hawajarejea kazini tangu walipoondoka, na
walitegemewa kurejea kazini tarehe 27 mwezi huu, baada ya sherehe za
Christimas, lakini haikuwa hivyo na kusababisha sintofahamu hiyo.
0 comments:
Post a Comment