Bunge la Uganda
limepitisha azimio la kupiga marufuku kuwasafirisha wasichana na wanawake wa
nchi hiyo katika nchi za nje, ili kufanya kazi kama watumishi wa ndani, kufuatia
kuwepo kwa matukio ya kufanyiwa ukatili na waajiri wao.
Katazo hilo linatokana na
taarifa ya iliyowasilishwa bungeni na Waziri wa Nchi anayehusika na Wazee
pamoja na Walemavu, Sulaiman Madada, iliyosema serikali inafahamu malalamiko
ya ukatili wananchi wa Uganda wanaofanyakazi za watumishi wa ndani katika nchi za Uarabuni.
ya ukatili wananchi wa Uganda wanaofanyakazi za watumishi wa ndani katika nchi za Uarabuni.
Wakati wa mjadala wa hoja
hiyo wabunge waliishutumu serikali kwa kuwatelekeza wananchi wa Uganda, wasio
na matumaini ya ajira, na kujikuta wakitegemea ukarimu wa makampuni 24
yaliyosajiliwa kuwatafutia ajira nchi za nje.
0 comments:
Post a Comment