Image
Image

Kenya kukabiliwa na mgomo kufuatia tishio la walimu na watumishi wa umma kugoma.




Nchi ya Kenya huenda ikatumbukia kwenye mgogoro mkubwa katika mwaka mpya utakaositisha shughuli za serikali, kufuatia tishio la walimu na watumishi wa umma kugoma kutoa  huduma ili kushinikiza kupewa posho zao.
Katibu Mkuu wa chama cha wafanyakazi Kenya, Wilson Sossion, jana ameumandikia Waziri wa Kazi Bw. Kazungu Kambi kumtahadharisha kuwa atawaongoza walimu na watumishi wengine wa umma kufanya mgomo mkubwa mwezi ujao, iwapo serikali haitaondo mafao yaliyopendekezwa na Tume ya Mishahara na Marupurupu, ifikapo jumatano wiki ijayo.
Bw. Sossion amesema zaidi ya watumishi wa umma 600,000 wakiwemo walimu, hawatorejea kazini Januari mwakani hadi hapo serikali itakapoondoa posho hizo alioziita duni zilizopendekezwa na tume na kuanzisha mchakato wa kujadiliana na watumishi kuhusiana na suala hilo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment