Image
Image

Muswada wa usalama wachafua bunge la kenya na kulazimika kuhairishwa.





Bunge la Kenya leo limelazimika kuahirishwa mara mbili baada ya kuibuka kwa vurugu ndani ya bunge hilo na kushindwa kujadili mapendekezo ya muswada wa sheria ya usalama.
Spika wa Bunge hilo Justin Muturi aliahirisha kikao hicho kwa dakika 30 lakini baadae vuruguu hizo zilibuka tena majira ya saa tano asubuhi na Spika kulazimka kuahirisha kikao hicho tena, huku wabunge wanaopinga muswada huo wakisikika wakiimba na kurusha 
karatasi sakafuni na kuvuruga mwenendo wa bunge.
Wakati huo huo idadi kubwa ya Askari polisi imetanda maeneo la jengo la Bunge la Kenya na mitaa iliyojirani na jengo hilo kuimarisha ulinzi kufuatia taarifa za kuwepo kwa maandamano ya kupinga muswada huo wenye utata.
Polisi wa kutuliza ghasia wakiwa na vifaa vyao wamewekwa katika lango kuu la bunge hilo Mtaa wa Harambee kuanzia alfajiri ya saa kumi na moja mapema leo tayari kupambana na maandamano yatakayoibuka.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment