Hospitali ya Mountmeru inakabiliwa na uhaba wa damu, vifaa tiba na dawa kwa wagonjwa.
Hospitali ya mkoa wa arusha ya Mountmeru inakabiliwa na changamoto za upungufu mkubwa wa benki ya damu vifaa tiba na bahadhi ya dawa hali inayochangia kudumaza utoaji wa huduma kwa wagonjwa na kusababisha madhara hasa kwa wagonjwa wanahohitaji huduma za haraka wakiwemo majeruhi wa ajali na wajawazito.
Mganga mkuu wa mkoa wa arusha Frida Mokiti ametoa kauli hiyo hospitalini hapo wakati waumini wa kanisa la TANZANIA ASEBLIS OF GOD walipo peleka msaada wa vyandarua elfu mbili na mia saba vyenye thamani ya shilingi milioni ishirini na moja kwa ajili ya wagonjwa katika hospitali zote na mkoa wa arusha zahanati na vituo vya afya ili kupunguza tatizo la maambukizi ya ugonjwa wa malaria kwa wagonjwa waliyopo hospitalini.
Akizungumza katika zoezi hilo askofu msaidizi wa kanisa LA ASEBILES OF GOD TANZANIA, Magnus Mhiche amesema kanisa linaguswa na matatizo yanayowapata wagonjwa ambao wengi wao ni watu wasiyo na uwezo huku bahadi ya watu wakiwa wanatumia fedha za umma kinyumme na mahitaji ya wananchi.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa arusha Daud Ntibenda amesema serikali ya mkoa wa arusha inafanya juhudi za kujikwamua na kero hiyo lakini hali bado ni mbaya na inatishia uhai wa wakazi wa arusha huku akiwataka wabunge kuunga mkono jududi za wadau kusaidia wananchi wanateseka na magonjwa ambao ndiyo waliyo waweka madarakani.
0 comments:
Post a Comment