Maghala
matano ya kiwanda cha maunt meru Oil Miller cha mjini singida kimeteketea kwa
moto na kuunguza zaidi ya tani elfutatu za mashudu ikiwemo mashine ya kukamulia
mafuta na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha.
Akieleza
mkuu wa mkoa wa singida Dk.Parseko Kone amesema kiwanda hicho ambacho kimeanza kuungua
majira ya saa tano usiku wa tarehe ishini natatu hadi sasa,imebidi mkoa kuomba
gari lingine kutoka mkoa wa jirani wa manyara ili kuweza kusaidia kuzima moto ambao
bado unaendelea kuwaka.
Kwaupande wake kamanda wa polisi mkoa wa
singida kamishina msaidizi wa jeshi la
polisi Bwana Thobias Sedoyeka amethibitisha kuungua kwa kiwanda hicho na jeshi la polisi limejitahidi kuweka
ulinzi na amewataka wananchi kutoa taarifa mapema pindi
matukio kama hayo yanapo tokea.
Meneja wa kiwanda hicho Bwana Sajay
Sumarzya amesema wao walipata taarifa
kutoka kwa walinzi usiku majira ya saa tano
na walipo fika walikuta maghala matano ya mashudu yenye tani zaidi ya elfutatu yakiwaka moto.
Hasante kwa kutuelimisha
ReplyDelete