Moto mkubwa
umeteketeza sehemu ya kiwanda cha kutengeneza magodoro kilichoko eneo la
mkuyuni jijini mwanza na kusababisha hasara ya mamilioni ya shilingi, huku
ajira za wafanyakazi zaidi ya 100 wa kiwanda hicho zikiwa katika hatihati ya
kusimama kwa muda usiojulikana.
Moto
ulioteketeza kiwanda hicho cha vitanda manufacturing company limited,
kinachomilikiwa na kundi la makampuni ya hashamjamal, ulianza majira ya saa
1.30 usiku na kufanikiwa kuzimwa saa 6
kwa msaada wa vikosi vya uokoaji na zimamaoto vya halmashauri ya jiji la
mwanza na uwanja wa ndege wa mwanza, ambapo baadhi ya mali yakiwemo magogoro,
majengo, mitambo pamoja na magari yaliungua huku baadhi ya nyaraka zikiteketea
na kubaki majivu.
Uongozi wa
kiwanda hicho kupitia kwa afisa masoko jayesh joshi umesema chanzo cha moto huo
ni hitilafu ya umeme huku ukishindwa kueleza thamani ya mali yote iliyoteketea.
Baadhi ya
watu walioshuhudia tukio hilo ambalo ni la pili kutokea katika kiwanda hicho
cha magodoro ya comfy, baada ya tukio la kwanza lililotokea mwezi oktoba mwaka
2006 wanaeleza mazingira yaliyopelekea kiwanda hicho kuungua.
0 comments:
Post a Comment