Wachimbaji
zaidi ya 200 kutoka maeneo tofauti ya ndani na nje ya mkoa wa tanga ambao
wanaodai kuwa wamepewa vibali vya uchimbaji na wizara ya nishati na madini
wamegomea agizo la serikali la kuwataka kuacha uchimbaji katika eneo la mgodi
wa kata ya kigongoi kwa sababu wanalipa kodi kwa serikali.
Akizungumza
katika mkutano wa dharura wa kujadili agizo la serikali uliofanyika katika
mgodi huo,mwenyekiti wa chama cha ushirika cha wachimbaji madini kata ya
kigongoi Augustino Hassan amesema hawataondoka katika eneno hilo hadi serikali
itakapokwenda kufanya tathmini ya uhalali wa kuchimba madini katika mgodi huo
kwa kushirikiana na wadau wa wizara ya nishati na madini pamoja na idara ya
misitu na nyuki mkoa wa tanga.
Baadhi ya wachimbaji wadogo waliokutwa katika
mgodi huo wamesema kitendo cha kuagizwa kuacha kuchimba madini kihalali hakina
lengo zuri kwa sababu makundi ya vijana wanaofuata sheria yakizuiwa kuacha
kufanya kazi hiyo yatakwenda kujikita katika vitendo viovu vya uporaji katika
jamii hatua ambayo ni ukiukwaji wa sheria za nchi.
ufuatia hatua hiyo mkuu wa wilaya ya mkinga
Bi. Mboni Mgaza amesema hatua hiyo ya kufunga mgodi huo imekuja kutokana na
uharibifu wa mazingira unaofanywa katika mgodi huo sanjari na kufanya ukaguzi
wa wachimbaji wenye leseni ili utaratibu mpya uweze kufanywa kisheria kwa lengo
la kuepuka vitendo vya uharibifu wa vyanzo vya maji yanayotumika na wakazi wa
tarafa ya maramba.
0 comments:
Post a Comment