Meja Jeneral Herman Corner
Mwili wa
aliyekuwa Meja Jeneral Herman Corner Lupogo aliyefariki 19 mwezi huu wa kumi
unatarajiwa kuagwa kesho katika eneo maalumu la Hospitali kuu ya jeshi lugalo
jijini Dar es salaam.
Marehemu
lupogo alijiunga na hi la ulinzi la wananchi wa tanzania julai 23 mwaka 1965
na hivyo kuweza kutunukiwa kamisheni januari 21 mwaka 1966.
Katika
utumishi wake enzi za uhai wake alifanikiwa kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo
ya mkurugenzi wa mafunzo makao makuu ya jeshi 1971 hadi 1974, katibu msaidizi
makao makuu ya chama (ulinzi na usalama) 1974 hadi 1976, mkuu wa chuo cha taifa
cha uongozi (monduli) 1976 hadi 1978.
Marehemu
meja jeneral lupogo nimzaliwa wa mkoa wa ruvuma na amezaliwa desember 12 mwaka
1938 wilayani mbinga mkoani ruvuma, na katika elimu yake aliyoipata aliweza
kuhitimu stashahada ya ualimu na shahada ya kwanza ya sanaa katika chuo kikuu
cha makerere nchini uganda mwaka 1958
hadi 1964.
Katika
utumishi wake alihudhuria kozi mbalimbali ikiwemo ukamanda na unadhimu nchini
canada 1969 na international strategic studies nchini uingereza 1985,na
amelitumikia jeshi kwa muda wa miaka 28.
Marehemu
amefariki akiwa mstaafu ameacha mke na watoto, Mwenyezi mungu ailaze roho ya
Meja Jenerali Hermani Corneli Lupogo (mstaafu) Roho mahali Pema Amina.
0 comments:
Post a Comment