Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge la
Katiba, Andrew Chenge amesema Katiba inayopendekezwa imebeba asilimia 75 ya
maudhui ya Rasimu ya iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Chenge
alitoa kauli hiyo jana mjini Dodoma alipokuwa akihitimisha michango ya hoja za
wajumbe wa Bunge hilo na kamati waliyoitoa wakati wa kuhakiki Rasimu ya Katiba
hiyo.
“Bunge
hili limeboresha Rasimu ya Katiba vizuri sana. Rasimu hii imebeba asilimia 75
ya maudhui ya Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba (Joseph) na nyie wajumbe
mmeboresha kwa asilimia 25 tu,” alisema Chenge.
Chenge,
ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), aliwataka wajumbe na
wananchi wasidanganywe na tafsiri zinazotolewa pembeni baada ya Mahakama kutoa
hukumu yake.
Katika
hukumu iliyotokana na kesi iliyofunguliwa na mwandishi wa habari, Saed Kubenea,
Mahakama ilitamka kuwa Bunge la Katiba lina mamlaka ya kuboresha na kurekebisha
rasimu ya Tume.
“Maoni ya
wananchi yamezingatiwa kwa kiwango cha juu sana na matumaini ya Watanzania juu
ya Katiba hii ni makubwa. Mambo yao yanayowagusa yamezingatiwa,” alisema.
0 comments:
Post a Comment