Dodoma.
Wajumbe wa Bunge la Maalumu la Katiba jana
walianza kupiga kura za kuamua ibara za Katiba inayopendekezwa, huku kura za
wajumbe kutoka Zanzibar zikiibua wasiwasi wa iwapo theluthi mbili itapatikana
au la.
Dalili za
kupiga kura za hapana kutoka upande wa Zanzibar zilianza kujionyesha mapema
baada ya taarifa za ndani kueleza kuwa zikikosekana 10 kutoka upande huo wa
Muungano hakuna katiba.
Hata
hivyo, mapema Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta alisema idadi ya kura
zinazohitajika kukidhi theluthi mbili kwa upande wa Zanzibar ni 140 na jana
jioni waliokuwamo bungeni walikuwa 142.
Mjumbe wa
kwanza kufungua pazia kwa kura ya hapana alikuwa ni Adil Mohamed Adil aliyepiga
ibara zote 157 kwa sura ya kwanza hadi 10.
Wengine
waliopiga kura ya hapana kwa sura zote ni Dk Alley Soud Nasoro na Salma Said.
Waliopiga
kura za hapana ni Fatuma Mohamed Hassan na Jamila Abeid Saleh, huku baadhi ya
wajumbe wakipiga kura za siri.
Kwa upande
wake, Ali Omary Juma, alikubaliana na sura za 2, 4, 5 na 9 lakini akizikataa
sura za 1,3,6,7,8 na 10.
Kwa upande
wa Tanzania Bara, wajumbe Abia Nyabakari na Dk Ave-Maria Semakafu walipiga kura
za ndiyo kwa baadhi ya sura na zingine kuzikataa.
Mjumbe Ali
Keissy Mohamed aliushangaza ukumbi kwa kupiga kura ya ndiyo kwa sura zote
tofauti na wakati akiwa katika vikao vya kamati ambapo alikataa muundo wa
serikali mbili.
Watakaopiga
kura kwa faksi
Mwenyekiti
wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta jana alitangaza orodha ya wajumbe 22
wanaotarajiwa kupiga kura kwa njia ya faksi au mtandao wakiwa nje ya Bunge
hilo.
Katika orodha hiyo, akiwamo Mwanasheria Mkuu
wa Serikali (AG), Jaji Fredrick Werema, wajumbe tisa wako Saudi Arabia kwa
ajili ya Hijja, wawili India kwa matibabu, mmoja yuko masomoni Uholanzi na
wengine nje ya Dodoma lakini yuko hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment