Idara ya Uhamiaji nchini
imesema asilimia kubwa ya
matatizo yanayoikabili ni pamoja na mchakato
wa utoaji wa hati za
kusafiria na tatizo la wahamiaji
haramu ,yanatokana na uelewa mdogo wa
wananchi juu ya
majukumu ya idara
hiyo na ugumu unaojitokeza katika
utekelezaji.
Akizungumza katika mkutano wa
mwaka wa kikao cha Baraza la
Wafanyakazi wa idara
hiyo unaofanyika Jijini Arusha , Kaimu Kamishna Mkuu
wa Idara ya Uhamiaji, Bw ana Peniel Mgonja amesema,kwa
asilimia kubwa , matatizo hayo yanatokana na utamaduni
wa wananchi wengi , kutaka kupata
huduma kwa njia
za mkato na pia kutumia muda
mwingi kulalamikia mambo
ambayo utatuzi wake
uko ndani ya
uwezo wao.
Kuhusu tatizo la wahamiaji
haramu, Bwana Mgonja amesema
pamoja na kuchangiwa
na kuwepo kwa njia nyingi za panya
katika mpaka wa Tanzania na
majirani zake , pia linachangiwa na baadhi ya
wananchi kurubuniwa na kujikuta wakiwasaidia
wahalifu.
Akifungua mkutano huo , Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi,
Bwana Mbarak Abdulwakili
amewataka wateandaji
kujenga utamaduni wa
kuwaeleza wananchi ukweli
kwa mambo yanayowezekana na yasiyo wezekana ili
wasipoteze muda n a
kwa yale yaliyoko nje
ya uwezo wao wayafikishe mapema
panapohusika .
0 comments:
Post a Comment