Serikali
imewashauri wahitimu kujiajiri wenyewe badala ya kutegemea ajira kutoka
serikalini kwani inatambua ukosefu wa ajira nchini.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar ea
Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe.
Willium Lukuvi alipokuwa akifungua kongamano la mafunzo kwa wajasiliamali
wadogo wadogo.
Amesema kuwa vijana
wanatakiwa kuweka mkazo katika suala la ujasiriamali na kujihusisha na mafunzo
mbalimbali ya ujasiriamali ili kuwa na fursa mbalimbali kiuchumi.
“Mtazamo chanya, kujitambua, kuwa
wabunifu na kusema inawezekana vinachangia kuzidisha maendeleo binafsi hivyo
kila kijana afikirie kuwa anaweza” aliongeza Waziri Lukuvi.
Mbali na hayo Waziri Lukuvi alisema
kuwa vijana hawana mitaji ya kujiendeleza lakini taasisi za kifedha
zinauwezo wa kuwakopesha iwapo watakua na vitambulisho vya Taifa na anwani za
makazi hivyo kupelekea vijana kujiajiri.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
wajiri nchini Bw. Almasi Maige amewaasa wahitimu kuwa na mawazo chanya na
kufikiria zaidi kuhusu kujiajiri na si kusubiri kuajiriwa.
“Hakuna ujasiriamali rahisi,
inatakiwa kujitoa haswa kwa watu ama vijana wenye nguvu kama ninyi” aliongeza
Maige.
Hivyo kuwashauri vijana kuwa
wabunifu na kuanzisha shughuli zitakazosaidia kuongeza kipato na si kutegemea
kukopi kutoka sehemu nyingine.
Kongamano hilo lililoandaliwa na
kampuni ya Gilgal nchini yenye kauli mbiu isemayo “wajasiriamali wadogo
fursa zilizowazi” lenye lengo la kubadili fikra kwa vijana walio vyuoni kutumia
fursa zilizopo.
0 comments:
Post a Comment