Rais UHURU KENYATTA wa Kenya ametia saini muswada wenye utata wa
sheria ya kupambana na ugaidi
ambao wakati wa mjadala wake bungeni ulizusha vurugu na wabunge
kurushiana makonde,
Muswada huo ulipitishwa na Bunge katika kikao kilichokumbwa na
ghasia huku Wabunge wa upinzani
wakionya kuwa Kenya ilikuwa inageuka kuwa taifa la polisi huku
serikali ikisema inahitaji mamlaka zaidi ya kupambana na wapiganaji wa kiislamu
wanaotishia usalama wa nchi hiyo.
Kupitishwa kwa muswada huo na kutiwa saini kuwa sheria na Rais
KENYATTA kunakuja wakati wapiganaji
wa Somalia wa kikundi cha al-Shabaab chenye uhusiano na mtandao wa
kigaidi duniani al-Qaeda kikizidisha mapigano nchini Kenya na kuua watu 64
katika mashambulio mawili ya hivi karibuni kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo.
Mapema mataifa tisa ya nchi za magharibi yaliunga mkono sheria
hiyo lakini yakataka serikali ya Kenya iheshimu haki za binadamu huku wapinzani
wakisema sheria hiyo itawanyima watu uhuru na haki zao na
kuvibana vyombo vya habari.
0 comments:
Post a Comment