Image
Image

Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam yawateua majaji wa tatu kusikiliza maombi ya IPTL na PAP juu ya sakata la Escrow





Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imewateua majaji watatu kusikiliza maombi ya makampuni ya kuzalisha umeme ya IPTL na PAP ya kutaka kuzuia utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu kashfa ya akuanti ya Tegeta Escrow.
Maombi ya kesi hiyo ambayo yataanza kusikilizwa kesho Jijini Dar es Salaam yatasimamiwa na majaji hao watatu ambao ni Jaji kiongozi Augustine Mwarija, Jaji Gadi Mjemas pamoja na Jaji Stela Mugasha.
Kwa mujibu wa hati ya kesi hiyo, IPTL na PAP inadai kwamba kilichofanyika ndani ya Bunge ni kinyume cha Katiba ya Jamhuri na kina lengo la kugombanisha mihimili mitatu ya dola; yaani Bunge, Mahakama na Serikali.
Hati hiyo inadai kwamba maazimio ya Bunge yanakiuka Ibara ya 13(1) ya Katiba ya Tanzania inayosema watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanastahili kutendewa haki bila kubaguliwa.
Hati hiyo inadai kuwa maazimio ya Bunge pia yamevunja Ibara ya 13(3) ya Katiba ya Tanzania inayotaka haki za kila mtu zilindwe na kuamuriwa na Mahakama, ikiongeza pia kuwa Bunge limekiuka kifungu cha 6(a) cha Ibara ya 13 ya Katiba kinachosema kuwa kila mtu ana haki kusikilizwa na kukata rufaa au kudai haki zake kisheria; pamoja na kifungu cha 6(b) cha ibara hiyo kinachosema mtu atakuwa hana hatia hadi pale Mahakama itakapomkuta nan hatia.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment