Serikali ya
Zambia imelitetea shirika lake la habari ambalo limekuwa likilaumiwa kwa
kuonyesha upendeleo kwa baadhi ya wagombea urais kwenye uchaguzi wa Januari 20
nchini humo.
Shirika la Habari la Zambia ZANIS limekuwa
likilaumiwa na wapinzani na mashirika ya kijamii kwa kuweka vifaa vyake vya
matangazo kwenye uteuzi wa mgombea wa ugavana wa chama tawala Bw Edgar Lungu.
Tume ya uchaguzi ya Zambia imetaja hatua hiyo kama inayompa Bw Lungu nafasi
kubwa ya ushindi dhidi ya wapinzani wake na kusisitiza kuwa huduma hiyo
inatakiwa kutolewa kwa kila chama cha kisiasa. Hata hivyo msemaji wa serikali Bw Joseph Katema amepinga madai hayo na kusema kitendo hicho hakikukiuka sheria za uchaguzi kwa kuwa kaimu rais Bw Guy Scott alikuwa miongoni mwa watu waliomsindikiza Bw Lungu kuwasilisha makaratasi yake ya uchaguzi.
Jumla ya wagombea 11 wamejitosa katika kinyang'ang'anyiro cha urais wa Zambia kufuatia kifo cha rais wa zamani Bw Michael Sata Oktoba 28.
0 comments:
Post a Comment