Umoja wa mataifa umesema mlinda amani wa Umoja huo nchini Liberia anatarajiwa kuendelea na majukumu yake huku akipokea ushauri nasaha baada ya kupona ugonjwa wa Ebola.
Akizungumza mjini New York, msemaji wa Umoja huo Bw Stephane Dujarric amesema mlinda amani huo kutoka Nigeria ambaye aligunduliwa kuwa na virusi vya Ebola na kusafirishwa kwenda Uholanzi Desemba 6 kwa matibabu alirudi Liberia jana jioni na anatarajiwa kuendelea na majukumu yake.
Liberia ni moja ya nchi tatu za Afrika magharibi ambazo zimeathirika vibaya na mlipuko wa Ebola, nyingine ni Sierra Leone na Guinea. Mapema mwezi huu shirika la Afya duniani WHO lilisema jumla ya watu 18,603 wameambukizwa virusi vya ugonjwa huo na idadi ya waliokufa kwa ugonjwa huo ni 6,915.
0 comments:
Post a Comment