Image
Image

ACT Walaani nguvu kubwa iliyotumiwa na jeshi la polisi dhidi ya Mwenyekiti wa CUF Mtoni Mtongani.




CHAMA cha Alliance For Change and Transparance( ACT- Tanzania.) kikizingatia msingi wa utu na uzalendo kwa taifa,kime pokea kwa masikitiko tukio la kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF),Prof.Ibrahim Lipumba huko mtoni Mtongani Katika Wilaya ya Temeke. jijini Dar esSalaam jana
Msingi wa kukamatwa Prof Lipumba na wenzake ni kwa ajili ya kuadhimisha kumbu kumbu ya mauaji ya Watanzania Wenzetu yaliyofanywa na jeshi la Polisi miaka 14 iliyopita wakati watanzania hao wasio na hatia walipotumia haki yao ya kidemokrasia kufikisha ujumbe kwa serikali kwa njia ya maandamano.
Kama iliyokuwa miaka 14 iliyopita kwa jeshi la Polisi kushindwa kutumia weledi wa kazi yao na kujiepusha na mihemko ya kisiasa jana tena wameendeleza uoneu wao kwa watanzania katika jitihada za kuminya Demokrasia na kufikisha mawazo huru kwa watawala wetu kwa kisingizio cha uwepo wa tishio la Ugaidi.
Kwa kutumia hoja dhaifu na visingizio vilivyo jaa mihemko ya kisiasa jeshi la Polisi likajiingiza katika kuwakamata na kuwadhalilisha viongozi wa (CUF), lengo likiwa ni kuwatisha watanzania hasa wakati huu tunapoelekea katika uchaguzi mkuu wa Rais Madiwani na wabunge
Sisi ACT-Tanzania tunaofuata misingi ya haki na uwajibikaji tunalaani vikali matendo ya jeshi la polisi kutumia nguvu kupita kiasi wakati wa kukabiliana na viongozi wa kisiasa kama ilivyofanyika jana
Aina hii ya nguvu ya jeshi la Polisi kwa ajili ya kukilinda chama kilicho madarakani ndiyo iliyopelekea kuuawa kwa mwanahabari Daudi Mwangosi miaka miatatu iliyopita jambao ambalo hatupendi lijirejee kwa mtanzania Mwingine
Tunalitaka jeshi la Polisi litende haki kwa vyama vyote kwa kuacha uwanja huru wa kufanya siasa, hasa tukizingatia wakati huu wanapowazuia viongozi wa CUF na kuwaruhusu wa CCM kufanya mikutano sehemu mbali mbali nchini kwa njia ya maandamano
Mwisho tunatoa Pole kwa prof.Lipumba wanachama n viongozi wote wa Cuf waliokamatwa hapo jana
ACT TANZANIA TAIFA KWANZA.
Imetolewa leo 28/01/2015.
Mohmmed Massaga Naibu Katibu Mkuu ACT.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment