Morogoro Wagoma.
Na kwa taarifa ambazo tunazo
hadi sasa ingawa migomo inaendelea baadhi ya mikoa Morogoro napo yaelezwa kuwa
wafanya biashara wamegoma kufungua maduka yao
Kinara wa Mgomo wa Wafanya biashara apandishwa
kizimbani Dodoma Muda huu.
Kiongozi wa wafanya biashara
Bwana Johnson Minja aliyekamatwa na jeshi la Polisi jana tayari leo tarehe 28 amefikishwa katika Mahakama kuu kanda ya Dodoma akikabiliwa na makosa
mawili,1.kosa la uchochezi,2.Kuhamasisha wafanya biashara kukataa matumizi ya mashine za kieletronic za kutokla risiti
za EFDs.
Hata hivyo inaelezwa kuwa
baada ya kufikishwa mahakamani hapo kutokana na makosa ya awali aliyoelezwa ila
taratibu za dhamana zinafanyika ilikuweza kuachiliwa.Fuatana nasi katika habari
zetu tutakujuza kwa kila hatua.
Katika
Siasa: Lipumba hali mbaya,Mbatia alipuka Bungeni.
Mwenyekiti wa CUF
Prof.Lipumba Amekamatwa tena na jeshi la polisi baada ya kuachiwa muda mfupi uliopita
wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo imeelezwa kuwa hali
yake sinzuri na kakimbizwa hospitali baada ya Presha kupanda Gafla.
Prof.Hali yake imebadilika ghafla wakati akiwa katika mahakama kuu ya Kisutu Jijini Dar es
Salaam na hivyo kukimbizwa katika Hospitali ya UN kinondoni DSM.
Hata hivyo leo hii bunge lilishindwa kuendelea na shughuli zake za Bunge
kwa mujibu wa utaratibu na ratiba ya Bunge hilo na kulazimika kuahirisha
shughuli zake za bunge baada ya wabunge wa upinzani kusimama na kupiga kelele
kwa kutaka hoja ya Mh.James Mbatia ya kutaka bunge liahirishe shughuli zake za
kawaida za bunge kwa nia ya kujadili kitendo cha Mwenyekiti wa CUF
Prof.Ibrahimu Lipumba pamoja na viongozi waandamizi wa chama hicho kupigwa na
Polisi jana.
Baada ya Mh.Mbatia
kuwasilisha hoja hiyo Spika wa bunge alitaka serikali kutoa tamko kesho ili
kutoa fursa kwa wabunge kulijadili jambo hilo lililokataliwa na wabunge wa
upinzani wakitaka jambo liwezekanalo leo lifanyike leo ndipo hali ya hewa
bungeni na kelele nyingi za kutoelewana kutokea na kulazimu Spika makinda
Kuahirisha Bunge Hadi Jioni.
0 comments:
Post a Comment