Jeshi la polisi
limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa chama cha wananchi CUF waliokuwa wakiandamana kwa ajili ya kukumbuka ya mauaji ya wenzao waliofariki huko Pemba Mwaka 2001.Kwenye maandamano hayo
alikuwepo mwenyekiti wake Profesa Ibrahimu Lipumba ambapo inaarifiwa kwa amepata kipigo na
kuumia sehemu mbali mbali huku waandishi wa habari wakikutana na kadhia hiyo
hali ambayo imewafanya wafanye kazi zao kwenye mazingira magumu.Maandamano hayo
ambayo yalikuwa na wafuasi wa CUF yamefanyika Mtoni kwa azizi alli Temeke jijini
Dar Es Salaam ambapo wameshindwa kuendelea na maandamano hayo kutokana na nguvu
kubwa iliyotumika eneo hilo huku watu wakikimbia ovyio ovyio ili kujinusuru
ingawa inaelezwa wapo walio pata majera mbali mbali.Chanzo cha sakata hili hadi
kuzuiliwa na kupigwa na mabomu ya machozi.
Profesa Lipumba alikamatwa Dar es Salaam wakati akiongoza maandamano yaliyoanza ofisi
za chama hicho wilayani Temeke kwenda kwenye viwanja vya Zakhiem, Mbagala
ulikopangwa kufanyika mkutano huo wa hadhara.
Kwa mujibu wa taarifa iliyokuwa imetolewa na chama
hicho, maandamano hayo ilikuwa ni sehemu ya kumbukumbu ya kuomboleza vifo vya
wana-CUF na wananchi wengine zaidi ya 70 waliouawa Zanzibar Januari 27, 2001,
wakati wa maandamano ya kupinga matokeo ya urais Zanzibar.
Chama hicho kilisema siku ya jana ilikuwa ni sehemu ya
kukumbuka mateso waliyofanyiwa wana-CUF waliondamana Tanzania Bara likiwemo
tukio la kuvunjwa mkono kwa Profesa Lipumba, wakati wa maandamano hayo. Pia bendera
zote za CUF siku ya jana zilipepea nusu mlingoti.
Wakati Polisi wakiwa wametoa amri ya kuzuia maandamano
hayo kutokana na kuwa na viashiria hatari, kulitokea malumbano baina ya wafuasi
wa CUF na Polisi.
Malumbano hayo yalianza baina ya maofisa wa CUF na
Polisi, kabla ya Profesa Lipumba kuwasili katika Ofisi ndogo za Chama hicho
zilizopo wilayani Temeke, ambapo polisi walikuwa wametanda kuhakikisha
maandamano hayo hayafanyiki.
Baada ya kuwasili Profesa Lipumba, malumbano pia yaliendelea
na pande zote kuonekana kutofikia mwafaka, lakini baadaye pande hizo
zilikubaliana maandamano yasifanyike badala yake waende viwanja vya Zakhiem kwa
magari yao.
Wakiwa kwenye magari baada ya kufika Mtoni Mtongani,
msafara wa Profesa lipumba uliokuwa ukiongozwa na Polisi ulikutana na kundi
kubwa la wapenzi na wanachama waliokuwa wamejipanga kumpokea kwa maandamano.
Hali hiyo iliwalazimu Polisi kuanza kufyatua mabomu ya
machozi kwa lengo la kuwatawanya wafuasi hao, huku Profesa Lipumba akishushwa
kwa nguvu kwenye gari alilokuwa amepanda na kuingizwa kwenye gari la polisi
kitemi, huku akionekana akilalamika kutokana na msukosuko aliokuwa anapata
wakati akiingizwa kwenye gari hilo.
Baada ya kuingizwa kwenye gari hilo, liliondoka kwa
mwendo wa kasi na kuacha wafuasi wake wameduwaa. Kamanda wa Operesheni Maalumu
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Saimon Sirro, alikiri kukamatwa kwa Profesa
Lipumba na kwamba taarifa kamili zitatolewa baadaye.
"Ni kweli Mwenyekiti Lipumba tunamshikilia lakini
kwa sasa ni mapema kutoa taarifa, hivyo subiri hadi baadaye tutatoa taarifa
rasmi," alisema Kamanda Sirro.
Mkurugenzi wa mipango na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa
CUF, Sheweji Mketo, alisema kuwa Chama hicho kiliomba kibali cha kufanya
maandamano hayo ambayo wanafanya kila mwaka kwa lengo la kuwakumbuka Watanzania
ambao wengi wao walipoteza maisha katika vurugu za kisiasa Zanzibar na wengine
kukimbilia nchi jirani.
Alisema walishangazwa na kauli ya jeshi hilo ya kuzuia
maandamano hayo wakati wao walitoa taarifa ndani ya saa 48 kama utaratibu
unavyo elekeza.
"Chama cha Wananchi (CUF) tuna utaratibu wa kila
mwaka kwa mwezi na tarehe kama ya jana kuadhimisha kumbukumbu ya watu waliokufa
katika vurugu za kisiasa za mwaka 2001; hivyo lazima tufanye maandamano,"
alisema Sirro.
Alisema kuwa, Jeshi hilo lilipaswa kutoa taarifa
mapema kama wao walivyopeleka maombi ya kufanya maandamano, lakini wamesubiri
bado siku moja, tena jioni; huku saa za kazi zimekwisha ndio walipeleka majibu
ya kuzuia maandamano.
0 comments:
Post a Comment