Image
Image

Fainali za mataifa afrika, tunisia na cape verde hakuna mbabe, zambia yashindwa kuwazuia Congo


Fainali za kombe la Mataifa Afrika zilizoanza mwishoni mwa juma lililopita nchini Equatorial Guinea zimeendelea tena jana kwa kushuhudia Tunisia wakilazimishwa sare ya kufungana bao 1-1- na Cape Verde katika mchezo uliochezwa uwanja wa Ebebeyin wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 5,000 tu. 
Katika mchezo huo wa kundi B, Tunisia ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 70 mfungaji akiwa ni Ali Moncer.
Bao la kusawazisha la Cape Verde lilifungwa kwa mkwaju wa penati na Almeida Ramos katika dakika ya 77 ya mchezo huo.
Katika mchezo mwingine wa fainali hizo za kuwania kombe la Mataifa ya Afrika, Zambia nao walijikutwa wakibanwa na Congo DRC baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1. 

Pamoja na kutangulia kupata bao katika dakika ya pili tu ya mchezo huo kupitia kwa mshambuliaji wake Given Singuluma, haikutosha kuwafanya Zambia waondoke na pointi zote tatu muhimu katika mchezo huo, kwani Congo DRC walisawazisha katika dakika ya 66 mfungaji akiwa ni Bolasie. 

Huo ulikuwa mchezo mwingine wa kundi B ulioshuhudia sare ya bao 1-1.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment