Image
Image

Familia 18 na watoto 10 walala nje kwa siku 23 Manispaa ya morogoro


Na.Mwandishi Maalum,Morogoro. 
Familia ya watu 18  wakiwemo watoto 10  wa kata ya mwembesongo manispaa ya morogoro wameendelea kulala nje  kwa siku 23 sasa huku wakinyeshewa mvua  kufuatia  kufukuzwa  kwa  nguvu  kwenye nyumba waliyokuwa wanaishi na  kuiomba serikali  iwasaidie.

Watu hao wengiwao wakiwa ni watoto bado wanaendelea kuteseka  na hali ngumu wanayoipata kwa kulala nje na kunyeshewa na mvua ambapo wakiongea kwa uchungu  huku wakionyesha hati halali ya umiliki wa nyumba yao  wameiomba serikali kuwasaidia ili kuondokana na hali hiyo.


Baba mzazi wa familia  ambaye anadaiwa kuuza nyumba hiyo Fredinandi Kainyingi amesema watoto wake ndiyo wamiliki halali wa nyumba hiyo licha ya kutoa ushahidi wa kutosha juu ya umiliki wa nyumba lakini vyombo vinavyohusika bado vinawanyima haki  na kushindwa kujua nini hasa lengo la vyombo. 

Aidha mwenyekiti wa mtaa wa Juma Hamsini Omari Makiluka na majirani wamesema wanajitahidi kuwapa misaada ya chakula ingawa hawanauwezo wa kuwapa huduma ya ladhi  watu wote hao na wameimba serikali  na mashirika ya haki za binadamu kuingilia kati kuona uwezekano wa kuwasaidia.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment