Hospitali
teule ya wilaya ya Sumbawanga inakabiliwa na msongamano wa wagonjwa na kusababisha watoto wadogo kulazwa wodi moja na watu
wazima na wakati mwingine watoto watatu
kutumia kitanda kimoja .
Mganga
Mfawidhi wa hospitali hiyo D akta AARON
HYERA amesema hayo wakati
akipokea msaada wa vifaa tiba
, vitanda na mashuka vilivyotolewa na Mfuko wa Pensheni
ya Watumishi wa U mma wa PSPF .
Amesema hospitali i nafanya juhudi ya
kukabiliana na tatizo hilo kwa kujenga wodi
nyingine kwa ajili ya watoto na wajawazito
ambapo zaidi ya shilingi milioni tisini zinahitajika ili kuikamilisha.
Akizungumzia hali hiyo, Katibu Tawala wa
Mkoa wa R ukwa Bwana SYMTHIES PANGISA akipokea msaada huo, amesema
serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kuboresha huduma
za kijamii za afya, elimu na maji na kuwapa wataalamu wa afy a wanaolipwa
mshahara na stahilk zote na serikali
kuu.
0 comments:
Post a Comment