Jeshi
la polisi nchini linawashikilia vijana 36 wa kundi maarufu Panya Road
wanaodaiwa kufanya vurugu na kupora mali za watu na kusababisha taharuki katika
jiji la Dar es salaam huku baadhi ya wananchi wakitoa maoni tofauti kuhusiana
na tukio hilo.
Akitoa
ufafanuzi wa taharuki hiyo msemaji wa jeshi la polisi SSP ADVERA BULIMBA ambaye
mbali na kuwatoa hofu wananchi kuwa hali hiyo haitajitokeza tena amesema jeshi
hilo limejipanga vizuri kukabiliana na vikundi vyovyote vinavyotaka kuvuruga
amani ya nchi na kwamba endapo polisi wasingewadhibiti vijana hao mapema tangu
wakiwa makaburini baada ya kumzika mwenzao aliyeuwawa na wananchi baada ya
kuiba hali ingekuwa mbaya zadi.
Kufuatia
tukio hilo TAMBARARE HALISI imezunguka maeneo mbalimbali ya jiji yaliyodaiwa kukumbwa na
tafrani hiyo ambapo baadhi ya wananchi wa maeneo ya magomeni ambako vurugu
zilianzia wameelezea namna zilivyoanza hadi kusababisha watu kuanza kukimbia
hovyo na wengine kuacha maduka yao wazi
na taarifa kusambaa maeneo mengine.
Katika
maeneo ya mwananyamala na ubungo baadhi ya waliozungumzia sakata hilo wameitaka
serikali kuangalia makundi ya vijana na ikiwezekana wapatiwe elimu ya
ujasiriamali bure ili waweze kuendesha maisha huku wengine wakishauri vijana
wasiokuwa na kazi mitaani wapelekwe jeshini wakafundishwe stadi za kazi pamoja
na uzalendo ili kuepuka vitendo hivyo.
Taharuki hiyo ilitokea usiku wa tarehe
mbili chanzo kikiwa ni kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la MOHAMED AYUB kuuwawa
na wananchi tarehe mosi mwaka huu katika maeneo ya tandale kwa mtogole kwa
tuhuma za wizi ambapo tarehe 2 maziko yalifanyika na taarifa zilizolifikia
jeshi la polisi zilidai kuwa baada ya maziko vijana wenzake walijipanga kufanya
fujo ili kulipiza kisasi.
0 comments:
Post a Comment