Image
Image

Kamati kuu ccm yakubaliana na Maazimio 8 ya bunge kuhusu Escrow.


Na.Mwandishi Wetu


Kamati kuu ya chama cha mapinduzi CCM,imkubaliana na maagizo nane ya bunge kuhusiana na sakata la akaunti ya  ya fedha ya tegeta escrow na kuiagiza serikali kutekeleza maadhimio ya bunge kama ilivyopendekezwa na kuwataka walewote walioopewa dhamana ya uongozi kuwajibika katika nyazifa zao kwa kuzingatia maadili. Katibu wa NEC na itikadi ya chama cha mapinduzi CCM Bwana NAPE NAUYE anajitokeza mbela ya wandishi wa habari  na kuelezea maadhimio ya kikao hicho kilichoketi mjini zanzibar na kuongozwa na mwenyekiti wake ambaye ni  Rais wa jamuhuri ya mungano wa tanzania DKT JAKAYA KIKWETE.

kuhusu adhabu iliyokuwa imewekwa na chama hicho kwa waliotangaza nia ya kugombea nafasi ya uraisi katika  uchaguzi wa mwaka 2015,bwana nape amesema kuwa kamati imeiagiza kamati ndogo ya maadili kuketi tarehe 19  january ili kutathimini adhabu hiyo na utekelezaji wake na kuleta maadhimio ya kamati ndogo ya maadili kwa  kamati kuu itakayoketi mwezi febr kuyapitia.

Aidha sakata la ununuzi wa mahindi toka kwa wakulima kaamti imeiagiza serikali kupitia upya mfumo wa ununuzi  wa mahindi toka kwa wakulima ili kuhakikisha kuwa wakulima wanapata stahiki zao.

kikao hicho cha kawaida kilichoketi mjini zanzibar kikiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho ambaye ni raisi wa jamuhuri ya mungano wa tanzania,kilichodumu kwa masaa nane na kutoka na maazimio manne ikiwemo sakata la escrow,hali ya kisiasa na mambo mengine ambapo watuhimiwa sita waliokuwa kwenye kifungo hicho cha chama cha mapinduzi ni mh: stiven wassira,wiliamu ngereja,january makamba,fredrick sumaye,edward lowasa na bernad membe.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment