Wanajeshi wa Kenya jana waliwauwa watuhumiwa
watano wa Kundi la Al-Shabaab katika mji wa pwani wa Lamu karibu na mpaka wa
Kenya na Somalia.
Msemaji wa jeshi la nchi hiyo kanali David
Obonyo amesema waasi walivamiwa na jeshi la Ulinzi la Kenya linalofanya kazi
chini ya jeshi wa tume ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika AMISOM, baada ya
kutambua eneo lililotaka kuvamiwa umbali wa kilomita 6 hadi Basuba Kaunti ya
Lamu.
Msemaji huyo pia amefafanua kuwa baadhi ya
wanamgambo wamekimbia wakiwa na majeraha, na operesheni ya kuwasaka ilianza
mara moja.
Kanali Obonyo amesema katika tukio hilo
wamepoteza mwanajeshi mmoja na wengine watatu waliojeruhiwa wanapatiwa
matibabu.
Wanamgambo wamekuwa wakijificha katika maeneo
ya msitu wa Boni ambako wanafanya mashambulizi dhidi ya wakazi na pia kuvamia
mabasi kwenye mpaka na Somalia.
0 comments:
Post a Comment