DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL
COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
Tanzania.
|
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili Maputo, mji mkuu wa Mozambique,
usiku wa Jumatano, Januari 14, 2015, kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais
mpya wa nchi hiyo, Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi.
Sherehe zinafanyika Independence Square, mjini
Maputo leo, Alhamisi, Januari 15, 2015. Mheshimiwa Nyusi anakuwa Rais wa nne wa
Mozambique tokea uhuru wa nchi hiyo mwaka 1975.
Kiongozi mwingine mkuu wa Tanzania aliyealikwa
kuhudhuria sherehe hizo ni Rais wa Tatu wa Tanzania, Mheshimiwa Benjamin
William Mkapa, ambaye amewasili akifuatana na mkewe, Mama Anna Mkapa.
Ujumbe wa Tanzania kwenye sherehe hizo ni pamoja
na Mama Salma Kikwete, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mheshimiwa Mahadhi J.Maalim,
Mheshimiwa Mohamed Abood Mohamed ambaye
ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Philip Mangula ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa
CCM, Mheshimiwa John Magale Shibuda
ambaye ni Mbunge wa CHADEMA na Mheshimiwa Halima Dendegu ambaye ni Mkuu wa Mkoa
wa Mtwara.
Imetolewa
na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
15
Januari,2015
0 comments:
Post a Comment