Walioona kibonzo hicho wanasema Mtume
Mohammad ataonekana akishikilia bango lililoandikwa "Je suis Charlie"
maneno yenye tafsiri "mimi ni Charlie, yaliyotumika kuonyesha mshikamano,
baada ya shambulizi katika ofisi za gazeti hilo jumatano wiki iliyopita ambapo
wafanyakazi kumi na wawili wa gazeti hilo waliuawa.
Nakala milioni tatu za gazeti hilo la kesho
tayari zimeshachapishwa tofauti na kawaida ambapo huwa linachapisha nakala
sitini elfu kwa wiki.
Source:BBC


0 comments:
Post a Comment